viongozi wachache wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo
Watu umeanza kukusanyika katika mji mkuu wa Iran Tehran kwaajili ya mazishi ya marehemu Rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi.
Bw Raisi alifariki pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na wengine sita katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili karibu na mpaka na Azerbaijan.
Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ataongoza sala katika mji mkuu, kabla ya majeneza yaliyofunikwa bendera ya Iran kupelekwa katika uwanja mkuu wa Azadi mjini humo.
Mamlaka imeonya dhidi ya maandamano ya kupinga mazishi hayo na ujumbe wa matusi mtandaoni.
Kote katika mji mkuu, mabango makubwa yamewekwa yenye ujumbe wa kumsifu Bw Raisi kama "mfia dini", huku mengine yakimuaga "mtumishi wa watu wasiojiweza".
Runinga ya serikali ilionyesha mitaa iliyojaa waombolezaji, wengi wao wakiwa wamebeba picha za Bw Raisi au bendera ya Iran.
Pia, viongozi wachache wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo.