Icj: un kutoa uamuzi juu ya wito wa israeli kusitisha harakati za kijeshi

Mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa inaweza kutoa hatua za dharura kuiamuru Israel kusitisha operesheni zake za kijeshi huko Gaza.

Kikao cha Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) siku ya Ijumaa ni sehemu ya kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini inayodai kuwa Israel inafanya mauaji ya halaiki.

Nchi zote mbili zilitoa ushahidi wakati kesi hiyo ilipofunguliwa wiki mbili zilizopita. Israel imekanusha vikali madai hayo.

Uamuzi dhidi ya Israeli hautekelezwi na mahakama lakini utakuwa muhimu kisiasa.

Zaidi ya Wapalestina 25,000 - wengi wao wakiwa wanawake na watoto - wameuawa na makumi ya maelfu kujeruhiwa, kwa mujibu wa wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza, tangu Israel ilipoanza mashambulizi yake, yaliyosababishwa na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa dhidi ya Israel na kundi hilo.

Shambulio la Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba liliua takriban watu 1,300, haswa raia. Washambuliaji hao pia waliwachukua takriban watu 250 na kuwapeleka Gaza kama mateka.

Afrika Kusini, ambayo inaunga mkono vikali Wapalestina, iliiomba mahakama hiyo kutoa masharti tisa ya muda, ikiwa ni pamoja na kusimamisha shughuli za kijeshi na Israel, huku ikizingatia tuhuma za mauaji ya halaiki.



Share: