Hospitali ya rufaa ya mkoa temeke (trrh) imeendesha zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi kwa kupima magonjwa yasiyo ya kuambukiza

lengo la kujenga uelewa juu ya umuhimu wa upimaji wa afya kwa jamii na kwa watoa huduma huku likilenga kufikia asilimia 95 ya watumishi

Idara ya Magonjwa ya Ndani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke (TRRH) imeendesha zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi kwa kupima magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Zoezi hilo limehusisha upimaji wa presha, sukari, pamoja na uwiano wa uzito na urefu, kwa lengo la kujenga uelewa juu ya umuhimu wa upimaji wa afya kwa jamii na kwa watoa huduma huku likilenga kufikia asilimia 95 ya watumishi. 

Uongozi wa hospitali unatambua umuhimu wa watumishi wa afya kuwa na afya bora, hivyo upimaji wa afya kwa watumishi wao ni moja ya jitihada za kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora kutoka kwa watoa huduma wenye afya imara.

Share: