Hezbollah yasema iliidungua ndege isiyo na rubani ya israel

Kundi la Hezbollah lenye makao yake makuu kusini mwa Lebanon, limetangaza kuwa liliidungua ndege isiyo na rubani ya Israel - mara ya kwanza kutoa madai hayo wakati wa mapigano ya hivi majuzi.

Kundi la Hezbollah lenye makao yake makuu kusini mwa Lebanon, limetangaza kuwa liliidungua ndege isiyo na rubani ya Israel - mara ya kwanza kutoa madai hayo wakati wa mapigano ya hivi majuzi.

Ilitokea siku ya Jumapili juu ya Khiam, kama kilomita 5 (maili 3) kutoka mpaka na Israeli.Ndege hiyo isiyo na rubani ilionekana ikianguka katika eneo la Israel, Hezbollah ilisema.

Kwa mujibu wa shirika hilo, ambalo limetajwa kama kundi la kigaidi na Uingereza na Marekani, wapiganaji wake 46 wameuawa katika mapigano na Israel tangu shambulio la Oktoba 7 la Hamas, pamoja na 43 kujeruhiwa.

Hezbollah pia inasema imeanzisha mashambulizi 84 katika maeneo 42 mpakani katika mapigano ya kila siku na wanajeshi wa Israel.

Israel inasema kuwa takriban wanajeshi wake saba wameuawa kufikia sasa

Share: