Geneva ni jiji la pili kwa ukubwa nchini Uswizi. Mji huo ambao wakazi wake wanazungumza Kifaransa
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton aliita Arusha "Geneva of Africa" yaani Geneva ya barani Afrika. Haikuwa kwa bahati mbaya na alifanya hivyo mwaka 2000 alipofika Arusha kushiriki mkutano wa kusaka amani ya Burundi na kubaini uzuri wa jiji hili muhimu kwa Afrika.
Geneva ni jiji la pili kwa ukubwa nchini Uswizi. Mji huo ambao wakazi wake wanazungumza Kifaransa unasifa ya kuwa "Jiji dogo Zaidi Duniani" na uko kwenye ukingo wa Ziwa Geneva, chini kabisa ya Milima ya Alps ya Uswizi.
Moja ya mambo ya kwanza ambayo watalii watahisi kuhusu Geneva ni utofauti wa kitamaduni. Geneva inajulikana kama "Mji Mkuu wa Amani", na ndipo kulipo na makao makuu ya mashirika zaidi ya 180 ya kimataifa.
Mikutano ya kimataifa, makongamano mengi ya kisayansi, maonesho tofauti kumeifanya Geneva kuwa jiji la kimataifa na lililotembelewa zaidi nchini Uswizi na kuiweka Geneva kwenye historia ya kudumu ya uvumilivu na utofauti.
Wakazi wa Arusha wanaamini mkuu wao wa mkoa Mh. Paul Makonda kama alivyofanikiwa Dar Es salaam hata pia Arusha inaweza kujengwa katika hadhi ile ya Geneva ya Afrika aliyoisema Rais Mstaafu Bill Clinton.