Gaza katikati mwa maadhimisho ya miaka 10 ya kifo cha mandela nchini afrika kusini

Vita vya Gaza vilikuwa kiini cha kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Nelson Mandela nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, huku maafisa wakuu wa Hamas wakihudhuria pamoja na familia ya shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi kwenye kumbukumbu hizo mjini mkuu Pritoria.

Maafisa wakuu wa Hamas walikuwepo: Basem Naim, waziri wa zamani wa afya wa Hamas huko Gaza, na Khaled Qaddoumi, mwakilishi wa kundi la wapiganaji wa Hamas kutoka Palestina nchini Iran. Katika siku zilizotangulia, walishiriki katika mkutano kuhusu mzozo wa Israel na Palestina mjini Johannesburg, ulioandaliwa hasa na mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela.

Kuundwa kwa taifa la Palestina kulizingatiwa na babu yake kama "swali kuu la maadili la wakati wetu", amekumbusha kwa idhaa ya kitaifa ya SABC, akisisitiza nia yake ya "kuchukua nafasi".

Afrika Kusini, mtetezi wa dhati wa kadhia ya Palestina, ni mojawapo ya nchi muhimu zaidi zinazokosoa na kulaani mashambulizi makubwa na mabaya ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza, kwa kulipiza kisasi mashambulizi ya umwagaji damu nchini Israel yaliyotekelezwa Oktoba 7 na Hamas. Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Mpakistani Malala Yousafzai, aliyealikwa Johannesburg na Wakfu wa Mandela, kwa upande wake alishutumu "mashambulizi yasio ya haki huko Gaza" wakati wa hotuba yake.

Share: