Gaza inazidi kuwa kaburi la watoto

Mamia ya wasichana na wavulana wanaripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kila siku

Gaza "inazidi kuwa kaburi la watoto", katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ameonya.

Akizungumza siku ya Jumatatu, António Guterres alionya kwamba hali katika eneo hilo "zaidi ya mgogoro wa kibinadamu, ni mgogoro wa ubinadamu".

"Mamia ya wasichana na wavulana wanaripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kila siku," Guterres aliambia mkutano wa waandishi wa habari, usiku wa kuamkia mwezi wa kwanza kamili tangu Hamas ilipoanzisha mashambulizi yake dhidi ya Israel, na jeshi la Israel likajibu kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Guterres alitoa wito tena wa kusitishwa kwa mapigano mara moja.

Matamshi yake yalikosolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen, ambaye aliandika "shame on you" kwenye mtandao wa X - ambao zamani ulijulikana kama Twitter – akiunganisha ujumbe huo na mkuu wa Umoja wa Mataifa.

"Zaidi ya watoto 30 - miongoni mwao mtoto wa miezi 9 pamoja na watoto wachanga na watoto ambao walishuhudia wazazi wao wakiuawa kikatili - wanazuiliwa kinyume na matakwa yao katika Ukanda wa Gaza," alisema na kuongeza

Share: