Finland yaimarisha uhusiano wa kijeshi na marekani

Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mahojiano na televisheni ya taifa, ameshtumu mataifa ya magharibi kwa kuiingiza Finland ndani ya NATO akitoa hoja kwamba Urusi imesululisha mizozo ya karne ya 20 na Finland.

Makubaliano hayo yanafanyika siku moja tu baada ya Rais Vladimir Putin kuionya Finland kwamba huenda ikapata "matatizo yasiyojulikana" kufuatia uamuzi wake wa kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO.

Mkataba huo wa ushirikiano wa ulinzi unapiga muhuri uhusiano wa Finland na Marekani, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya pamoja ya vikosi vya usalama sambamba na hatua ya Helsinki kujiunga na NATO mwezi Aprili.

Akitia saini makubaliano hayo mjini Washington akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, Waziri wa ulinzi wa Finland Antti Hakkanen amesifu makubaliano hayo na kuyataja kama ishara ya kujitolea kwa Marekani katika ulinzi wa Finland na eneo lote la Ulaya Kaskazini.

Share: