Familia za mateka wa israel zinataka kukutana na baraza la vita

Familia za mateka wanaoshikiliwa ndani ya Gaza zinasema wamekuwa na wasiwasi mkubwa usiku mzima wakati Israel ikifanya mashambulio makubwa katika eneo hilo.

Katika taarifa iliyotolewa asubuhi ya leo, familia hizo zinaomba kukutana na Waziri wa Usalama wa Israel na wanachama wa baraza la vita haraka iwezekanavyo.

“Huu ulikuwa  Usiku mbaya zaidi kuwahi kutokea. Ulikuwa ni usiku mrefu usio na usingizi, kufuatia oparesheni kubwa ya IDF ndani ya Gaza, na tulikuwa na wasiwasi sana kuhusu hali ya mateka wanaoshikiliwa ambao pia ni waathirika wa mashambulizi haya makubwa.”

Taarifa hiyo inasema oparesheni ya ardhini inahatarisha usalama wa Walsrael 229 wanaoshikiliwa ndani ya Gaza. Inaendelea kwa kusema: “Familia zina wasiwasi kuhusu hatma za ndugu zao na wanasubiri maelezo zaidi. Kila sekunde inavyopita ndivyo wasiwasi inavyozidi kuongezeka. Tunataka Waziri wa ulinzi Yoav Gallant na wanachama wa baraza la vita kukutana na sisi asubuhi ya leo!.”

Mapema hii leo, msemaji wa IDF amesema kuwa kuwarudisha watu waliotekwa ni “jitihada muhimu kwa nchi. Na hatua zetu zote, oparesheni, uchunguzi wa siri, unalenga kutimiza lengo hili.”

Share: