FAHAMU: MTOTO WA RAISI MUSEVENI ANA TATIZO NA BALOZI WA UJERUMANI

Wana Diplomasia baadhi wa ulaya walitoa malalamiko dhidi ya mtoto wa Raisi wa uganda , anae famika kwa majina Muhoozi Kainerugaba baada ya kuandika na kuchapisha maneno juu ya balozi wa Ujerumani aliopo sasa nchini Uganda.

Mtoto wa Raisi kainerugaba  ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa  X  " Tuna tatizo na balozi wa ujerumani aliopo sasa hapa uganda,Tatizo  linamuhusu yeye binafsi ,hana sifa bza kuwa hapa.Hili halihusiani na wananchi wa Ujerumaniambao na wathamini na ninawaheshimu."


Jeshi la uganda limetangaza kusimamisha ushirikiano wa kijeshi na Ujerumani,lilimshutumu Balozi wa ujerumani nchini humo, Balozi Matthias SChauer, kwa madai ya kuhusika katika vitendo ya uchochezi .UPDF ikadai kuwa  baadhi ya mabalozi kutoka Ulaya wamekuwa wakiunga mkono na kutumika na makundi ya upinzani.



Share: