Waraka huo wa kurasa 84 uliowasilishwa na Afrika Kusini unasema kwamba hatua za Israel "ni za mauaji ya halaiki kwa sababu zinataka kusababisha uharibifu wa sehemu kubwa" ya Wapalestina huko Gaza.
Alhamisi hii, Januari 11 na Ijumaa, Januari 12, mawakili wanaowakilisha Afrika Kusini na Israel watafika mbele ya mahakamani ya kimataifa ya haki.
Je, Israel inafanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza?
Afrika Kusini inasema ndiyo ndiposa ikawasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko The Hague mnamo Desemba 29, 2023.
Lakini Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema nchi yake inaishi kwa "maadili" yasiyo na kifani katika kampeni yake ya Gaza, wakati msemaji wa serikali alifananisha kesi ya Afrika Kusini na "kashfa ya damu," shutuma za uongo. kwamba Wayahudi waliwaua Wakristo ili kutumia damu yao katika desturi za kale.
Waraka huo wa kurasa 84 uliowasilishwa na Afrika Kusini unasema kwamba hatua za Israel "ni za mauaji ya halaiki kwa sababu zinataka kusababisha uharibifu wa sehemu kubwa" ya Wapalestina huko Gaza.
Inashikilia kuwa vitendo vya mauaji ya halaiki ni pamoja na kuwaua Wapalestina, na kusababisha madhara makubwa ya kimwili na kiakili, na kuweka kimakusudi masharti yaliyokusudiwa "kuleta uharibifu wao wa kimwili kama kikundi." Inasisitiza zaidi kuwa matamshi ya maafisa wa Israel yanaeleza nia ya mauaji ya kimbari.
Juliette McIntyre, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Australia Kusini, aliambia BBC kwamba ombi la Afrika Kusini ni "la kina sana" na "imetungwa kwa uangalifu sana."
"Inatafuta kujibu hoja zote zinazowezekana za Israel na kushughulikia madai yoyote ambayo mahakama inaweza kushughukia au kukosa mamlaka ya kufanya hivyo," alisema.
"Afrika Kusini inasema iliibua suala hilo na Israel katika majukwaa mengi tofauti kabla ya kuleta kesi hiyo,"
Msemaji wa serikali ya Israel Eylon Levy amesema Israel itatetea msimamo wake kuhusu kesi hiyo.
Pia alisema kuwa Hamas ndio inastahili kulaumiwa kwa kuanzisha vita vita hivyo.