EMINEM AIFUNGULIA MASHTAKA YA DOLA  MILIONI 109 KAMPUNI YA META

Kampuni ya uchapishaji wa muziki ya Rapa Eminem,Eight Mile style,imefugua kesi dhidi ya kampuni ya meta platforms,wamiliki wa facebook,Instagram,na whatsapp ikidai ukiukaji wa hakimiliki na kutaka fidia ya zaidi ya dola millioni 109 za kimarekani.

Kulingana na nyaraka za mahakama zilizowasilishwa mei 30 mwaka huu 2025,kampuni ya Eminem Eight Mile styles inadai kuwa Meta ilitumia nyimbo 243 kutoka kwenye orodha ya msanii nguli Rapa Eminem bila ruhusa,kupitia vipengele kama"original Audio" na "Reels Remix" bila leseni au kutaja chanzo husika (sahihi).Kampuni hiyo inasema nyimbo hizo zilitumika katika mamilioni ya video katika watumiaji wa Meta na kusababisha  hasara kubwa ya mapato.


Eight Mile Style inadai fidia ya dola za kimarekani zisizo pungua 150,000 kwa kila wimbo uliotumika bila ruhusa ,jumla ikiwa dolla milioni 109.35 kwa nyimbo 243 zilizotumika bure. Ingawa Meta ilijaribu  kupata leseni  kupitia kampuni ya Audiam,Eight Mile Style imesema haikuwahi kutoa ruhusa hiyo.Baadhi ya nyimbo ziliweza kuondolewa baada ya malalamikoya awali,lakini Meta inadaiwa kuendelea kuhifadhi na kusambaza nyimbo hizo bila leseni yan ruhusa.

Ipo wazi kuwa Msanii Eminem mwenyewe hajatajwa kama mlalamikaji katika kesi hii,Huku kampuni ya Meta bado haijatoa tamko rasmi kuhusu madai hayo.

Share: