Hukumu hii ni ya kwanza tangu kuondolewa kwa kusitishwa kwa adhabu ya kifo nchini DRC
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Wanajeshi wanane, wakiwemo maafisa watano, wamehukumiwa kifo kwa uoga na kuwakimbia maadui na Mahakama ya Kijeshi huko Goma, Mashariki mwa nchi.
Hukumu hii ni ya kwanza tangu kuondolewa kwa kusitishwa kwa adhabu ya kifo nchini DRC. Askari watatu waliachiliwa huru ambapo wote walikuwa wamepelekwa Kivu Kaskazini katika kupambana na waasi wa M23.
Kulingana na Mwendesha Mashtaka, mnamo Desemba 24, wanajeshi hao walipelekwa karibu na Saké, takriban kilomita 20 Magharibi mwa Mji Mkuu wa mkoa wa Goma, katika mapigano yaliyowahusisha Jeshi la Congo, washirika wake na M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na kisha wakawakimbia waasi, kwa mujibu wa Mahakama.
Mawakili na wateja wao sasa wana siku tano za kukata rufaa. Askari wengine watatu waliachiliwa huru.