Rapper kutoka marekani Drake anatajwa kufungua kesi dhidi ya record label yake ya UMG na Spotify kwa madai ya kupanga alichokiita upendeleo kwa kuhakikisha wimbo wa 'Not Like Us' wa Kendrick Lamar unakua juu.
Madai hayo ya Drake yanaeleza kuwa Rec label yake ya UMG imekua ikitumia mtandao wa Spotify na Apple Siri kuipandinsha Not like Us dhidi ya ngoma zake, kuwafukuza kazi wafanyakazi walikua wakionesha kumuunga mkono Drake na Kuwalipa watu wa media ili kuicheza sana ngoma hiyo, ambayo ilitoka kama diss Trake kwenda kwa kwake.