Msanii maarufu wa muziki, Drake, ametangaza kuondoa rasmi kesi yake dhidi ya Universal Music Group (UMG) na Spotify, akituhumu kampuni hizo kwa njama za kuboresha usikilizwaji wa wimbo wa Kendrick Lamar, "Not Like Us" kwa gharama ya kazi zake mwenyewe.
Katika hati ya mahakama iliyowasilishwa Jumanne, kampuni ya Drake, Frozen Moments, ilijiondoa kwenye maombi ya awali ya kupata nyaraka muhimu kutoka UMG na Spotify.
Hii ilikuwa ni sehemu ya uchunguzi wa madai kwamba ‘bots’ na malipo haramu yalitumika kupandisha kiwango cha usikilizwaji wa wimbo huo, ambao pia ulimhusisha Drake katika madai mazito ya kumdhalilisha.
Kwa upande wake, Spotify imekanusha vikali madai hayo, ikieleza kuwa hawakuwa na sababu za kiuchumi za kuipendelea kazi ya Lamar dhidi ya zile za Drake.
Hati ya upinzani ya Spotify ilieleza kuwa madai hayo ni ya "kupotosha" na hayana msingi wa kisheria.