Kupitia taarifa yake iliyochapishwa katika Mtandao wa X, Kiongozi wa Kisiasa wa kundi hilo, Bertrand Bisimwa amesema maeneo yaliyopata Viongozi ni kutoka Kivu Kaskazini ambayo ni Rutshuru, Kiwanja, Rubare na Bunagana
Kundi la Waasi la M23 limeripotiwa kutangaza Uteuzi wa Uongozi wake katika maeneo yaliyopo chini ya udhibiti wake huko Mashariki mwa DRC, hali inayodaiwa kuzua wasiwasi kwamba linapanga kuunda Taifa huru katika eneo hilo
Kupitia taarifa yake iliyochapishwa katika Mtandao wa X, Kiongozi wa Kisiasa wa kundi hilo, Bertrand Bisimwa amesema maeneo yaliyopata Viongozi ni kutoka Kivu Kaskazini ambayo ni Rutshuru, Kiwanja, Rubare na Bunagana
Ikumbukwe, M23 imejimilikisha eneo kubwa katika Mji wa Goma licha ya kukabiliana na mashambulizi makali kutoka Vikoshi vya Jeshi la DRC. Aidha, kundi hilo limekuwa likidaiwa kupata misaada ya kivita kutoka nchi jirani ya Rwanda ingawa, Serikali ya Kagame inakanusha taarifa hizo