Donald trump rais wa zamani wa marekani ameahidi kumaliza vita "ndani ya saa 24" ikiwa atachaguliwa

Donald Trump hatafadhili vita vya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi ikiwa atachaguliwa tena kuwa rais wa Marekani, Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema.

"Hatatoa hata senti katika vita vya Ukraine na Urusi, hivyo vita vitakwisha," Waziri Mkuu huyo wa kihafidhina alisema baada ya kukutana na Bw Trump huko Florida.

Rais wa zamani wa Marekani ameahidi kumaliza vita "ndani ya saa 24" ikiwa atachaguliwa - lakini hakutoa maelezo.

Bw Orban anaunga mkono waziwazi mshirika wake wa muda mrefu katika kinyang'anyiro cha 2024 White House."Ni dhahiri kwamba Ukraine haiwezi kusimama kwa miguu yake," Bw Orban aliambia kituo cha runinga cha Hungary cha M1 Jumapili.

"Kama Wamarekani hawatoi pesa na silaha, pamoja na Wazungu, basi vita vimekwisha. Na ikiwa Wamarekani hawatatoa pesa, Wazungu peke yao hawawezi kufadhili vita hivi.

Halafu vita vitaisha. "Aliongeza kuwa Bw Trump alikuwa na "mipango ya kina" kuhusu jinsi ya kumaliza vita vya Urusi na Ukraine - lakini hakufafanua.

Bw Trump hajatoa maoni yake hadharani kuhusu mahojiano ya runinga ya Bw Orban.Katika mkutano wao wa Ijumaa katika jumba la kifahari la Bw Trump la Mar-a-Lago, rais huyo wa zamani wa Marekani alimsifu mgeni wake.

"Hakuna mtu ambaye ni bora, nadhifu, au kiongozi bora kuliko Viktor Orban. Yeye ni mzuri," alisema.Katika ziara yake nchini Marekani, Bw Orban hakukutana na Rais wa sasa wa Marekani Joe Biden, ambaye anatarajiwa kuwa mpinzani mkuu wa Bw Trump katika uchaguzi wa urais mwezi Novemba.

Share: