Donald Trump na P Diddy wametafutwa zaidi 2024 kwenye mtandao wa google

Kampuni ya Google imetoa orodha ya Watu na vipengele mbalimbali vya maudhui yaliyotafutwa zaidi katika mtandao huo kwa mwaka 2024 ambapo Rais mteule wa Marekani, Donald Trump na Msanii mkongwe wa Marekani P Diddy wameongoza kwa kutafutwa zaidi kwa mwaka mzima.

Kulingana na ripoti ya kila mwaka ya Google, katika mwaka wa 2024 Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameongoza orodha ya Watu waliotafutwa zaidi katika mtandao huo akifuatiwa na Binti Mfalme wa Wales, Catherine, Kamala Harris, Imane Khelif n.k

Katika orodha ya Wasanii waliotafutwa zaidi katika Google 2024, Msanii mkongwe Diddy Combs ameongoza orodha hiyo kwa kutafutwa zaidi akifuatiwa na nyota wa RnB, Usher Raymond, Linkin Park, Sabrina Carpenter, Justin Timberlake, Angela Aguilar, Drake, Tracy Champman n.k.

Share: