Baada ya kushinda Kiti cha Urais wa Marekani, Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameendelea kuunda serikali yake mpya ambapo saa chache zilizopita ameunda Idara ya Ufanisi Serikalini na kumteua Elon Musk kuongoza Idara hiyo akiwa sambamba aliyekuwa mgombea Urais wa chama cha Republican Vivek Ramaswamy.
Donald Trump alisema maneno yafuatayo baada ya kufanya uteuzi wa kuwapa jukumu la kuongoza Idara mpya ya Ufanisi Serikalini. "Kwa pamoja, Wamarekani hawa wawili ( ElonMusk & Ramaswamy) wa pekee watafungua njia kwa Utawala wangu kufuta Urasimi Serikalini, kupunguza kanuni za ziada, kupunguza matumizi yasiyofaa, na kuunda upya Mashirika ya Umma".
Elon Musk alizaliwa Pretoria nchini Afrika Kusini Juni 28, mwaka 1971 (miaka 53 iliyopita) ambapo Mama yake ana asili ya Canada na Baba yake ni mzaliwa wa Afrika Kusini, Elon ndiye mmiliki wa SpaceX (Mtandao wa X zamani Twiter) na Tesla Inc. inayotengeneza magari ya Tesla. Kampuni za Elon Musk zimeonyesha mapinduzi makubwa katika nyanja za teknolojia ya anga. Elon Musk ni baba wa watoto 12. Elon Musk ndie tajiri namba 1 duniani kwa sasa.