Donald Trump amtaja tajiri Elon Musk kuwa ni nyota mpya ya Republican

Donald Trump katika Hotuba yake amtaja tajiri mmiliki wa makampuni mbalimbali kama Tesla na X twitter Elon musk kwasasa ndiye nyota mpya ya Republican

Baada ya shangwe na nderemo kutoka kwa umati uliokusanyika, Trump alianza kuzungumza juu ya mtu ambaye amekuwa sehemu muhimu katika kampeni yake - mmiliki wa mtandao wa X na mtu tajiri zaidi duniani Elon Musk. 



Alimtaja Musk kama "nyota mpya" wa Chama cha Republican, kabla ya kuendelea kusimulia hadithi ndefu kuhusu jinsi alivyomwacha bilionea huyo akiwa amesimama kwa dakika 40 wakati akitazama video ya roketi ya kampuni ya SpaceX.

Trump Musk anamtaja kama mtu "wa kipekee".

Tajiri huyo mkubwa zaidi duniani alikuwa na uhusiano mbaya na Donald Trump wakati Trump alipokuwa rais, lakini Musk ameelezea kutofurahishwa kwake na Democratic katika miaka ya hivi karibuni hasa wakati wa Uongozi wa Joe Biden na Kamala Harris. 


Kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa 2022, Musk alitangaza amekihama chama hicho na kuwahimiza wafuasi wake kuipigia kura Republican.

Mwaka huu, amejihusisha na siasa za Marekani, akitoa michango na machapisho ya mitandaoni kwa niaba ya Warepublican kadhaa.


Musk alizindua America PAC, Julai kwa lengo la kuunga mkono kampeni za Trump za kuwa rais. Hadi sasa amechangia takribani dola milioni 75 katika kikundi hicho, pesa ambazo zimekuwa zikigaiwa bure kwa Kila Mmarekani aliyekuwa amejiandikisha kwaajili ya kupiga kura hapo jana Jumanne.

Share: