Donald trump amemtangaza seneta wa jimbo la ohio, jd vance kuwa mgombea mwenza

Trump tayari ametangazwa rasmi kuwa Mgombea wa Urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican

RAIS wa zamani wa Marekani na Mgombea wa Urais wa Nchi hiyo kupitia Chama cha Republican, Donald Trump amemtangaza Seneta wa jimbo la Ohio, JD Vance kuwa Mgombea mwenza wake ambapo ikiwa Trump atashinda Urais basi JD Vance atakuwa Makamu wa Rais wa Marekani.


Trump tayari ametangazwa rasmi kuwa Mgombea wa Urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican baada ya kupata kura zinazotosha kuwa Mgombea.

Share: