Dkt. philip mpango apokea tuzo ya amani duniani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Mpango akipokea Tuzo ya Amani Duniani iliyotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Four Points by Sheraton Jijini Dar es salaam tarehe 20 Februari 2024. Tuzo hiyo imetolewa na Chuo kikuu cha Dar es salaam kupitia Kigoda cha Uprofesa cha Mwl. Julius Nyerere katika Kiswahili.

Share: