Dk. mwinyi akutana na rais wa msumbiji Mhe. filipe jacinto nyusi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema uhusiano uliopo kati ya Msumbiji na Tanzania ni wa ukaribu na urafiki. 


Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe: 4 Julai 2024, alipokutana na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi aliyefika Ikulu Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza ziara yake ya Kitaifa ya siku nne nchini. 

Aidha Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Rais Nyusi kwa kuitembelea Zanzibar. 


Kwa upande mwingine Rais Nyusi ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi pia, alitumia fursa hiyo kumwalika Rais Dk. Mwinyi kutembelea Msumbiji kabla ya kumaliza muda wake madarakani.

Msumbiji inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu wa Rais mwezi oktoba mwaka huu.

Share: