DIDDY AMEOMBA MHAKAMA ISITISHE MASHITAKA JUU YAKE KWA SABABU ZIFWATAZO

P. Diddy (jina halisi Sean John Combs) ni msanii wa muziki, mtayarishaji, mfanyabiashara, na mfanyaji wa filamu kutoka Marekani. Alizaliwa tarehe 4 Novemba 1969, mjini New York.

"Diddy" Combs, maarufu kama P. Diddy, anashikilia mashtaka makubwa ya jinai na madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia. Hadi Juni 2025, anashtakiwa kwa makosa kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

Mashtaka ya Jinai,Ushirikiano katika uhalifu wa kimataifa (racketeering conspiracy): Inadaiwa aliongoza mtandao wa uhalifu unaohusisha unyanyasaji wa kijinsia, utumwa wa kingono, utekaji nyara, na ulaghai.Uhamasishaji wa ushiriki katika ukahaba (sex trafficking): Anadaiwa kulazimisha wanawake kushiriki katika vitendo vya ukahaba.


Diddy ameomba mahakama isitishe kesi dhidi yake kwa madai kuwa ushahidi wa uongo uliwasilishwa.

Katika barua mpya iliyowasilishwa na mawakili wake, Diddy anadai upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa uongo kuhusiana na tukio linalomhusisha Bryana Bongolan.

Cassie, aliyekuwa mpenzi wake, alidai alimwona Diddy akimng’iniza Bryana juu ya balcony na kumtupa kwenye fanicha, lakini timu ya utetezi inasema hakushuhudia tukio hilo na ushahidi wa jumbe za simu unaonyesha aliambiwa na mtu mwingine.

Aidha, wanadai kuwa Bryana alitoa ushahidi wa uongo kuhusu tarehe na mahali pa tukio, huku serikali ikijua au ikipaswa kujua kuwa Diddy alikuwa katika Pwani ya Mashariki wakati huo.Usafirishaji kwa madhumuni ya ukahaba (transportation for prostitution): Anadaiwa kusafirisha wanawake kwa madhumuni ya ukahaba.

Share: