Dawasa imetangaza upungufu wa huduma ya maji kwa wateja

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetangaza upungufu wa Huduma ya Maji kwa Wateja wanaohudumiwa na mtambo Ruvu Chini, kuanzia Machi 5 hadi Machi 7, 2024 kutokana na maboresho yanayofanywa katika mtambo

Maeneo yatakayoathirika ni Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Goba, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi na Kijitonyama

Maeneo mengine ni Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.

Share: