Dart yasitisha safari za mabasi ya mwendokasi yanayopitia njia ya jangwani

Taarifa ya Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) maarufu kwa jina la Mabasi ya Mwendokasi ya Aprili 23, 2024 imesema Barabara ya Jangwani imefungwa kutokana na mafuriko, hivyo Mabasi kwa njia za Kimara hadi Kivukoni na Gerezani yataishia Magomeni Mapipa


Vilevile, huduma ya usafiri wa Mabasi ya DART inaendelea kutolewa kwa njia ya Morocco kwenda Kimara na eneo la katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa njia ya Muhimbili na Gerezani

Share: