Daktari bandia wa tiktok akamatwa katika hospitali ya afrika kusini

Mshawishi maarufu wa TikTok nchini Afrika Kusini ambaye alidai kuwa daktari amekamatwa, karibu wiki tatu baada ya mamlaka kumtuhumu kwa ulaghai.

Mshawishi maarufu wa TikTok nchini Afrika Kusini ambaye alidai kuwa daktari amekamatwa, karibu wiki tatu baada ya mamlaka kumtuhumu kwa ulaghai.

Matthew Lani alikamatwa na usalama wa Hospitali ya Helen Joseph ya Johannesburg alipokuwa akijaribu kuingia katika kituo hicho Jumapili usiku.

Idara ya Afya ya Gauteng ilisema kuwa timu ya usalama ya hospitali ilimsalimisha kwa polisi.

"Lani alinaswa kabla ya saa nane usiku akiwa amejifunika kofia na kuvaa barakoa ya upasuaji na stethoscope shingoni," idara hiyo ilisema katika taarifa.

Iliongeza kuwa Lani "hapo awali alikuwa ameingia katika kituo hicho ili kudhibiti maudhui ya kupotosha kwa kisingizio kwamba alikuwa daktari aliyehitimu".\

Lani alikuwa amejikusanyia mashabiki wengi kwenye TikTok, ambapo alichapisha maudhui ya matibabu na kuuza aina yake ya vidonge.

Alidai kuwa alihitimu udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand, jambo ambalo chuo hicho kilikanusha.

Pia alidai kuwa jina lake halisi ni Dkt Sanele Zingelwa, lakini alifichuliwa kuwa alijifanya kuwa daktari katika kituo kingine.

Baraza la Taaluma za Afya la Afrika Kusini lilisema kuwa Lani hakuwa daktari aliyesajiliwa

Share: