Cuba na tanzania kuongeza ushirikiano sekta ya elimu

Zaidi ya Watanzania 300 wamesoma Cuba, huku zaidi ya 200 kati yao wakisoma masomo ya udaktakari

Tanzania na Cuba zimekuwa zikishirikiana kwa ukaribu kwa zaidi ya miaka 60 sasa huku maeneo ya ushirikiano yakikua siku hadi siku na elimu ikiwa moja ya sekta zinazonufaika zaidi.

Jioni ya leo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba amekutana na Balozi wa Cuba anayeiwakilisha Tanzania, Balozi Yordenis Vera katika ofisi ndogo za wizara kujadili maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili pamoja na kutathmini mwelekeo wa ushirikiano wa Tanzania na Cuba katika sekta ya elimu.

Zaidi ya Watanzania 300 wamesoma Cuba, huku zaidi ya 200 kati yao wakisoma masomo ya udaktakari. Awali zilikuwepo na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania kusoma Cuba ambazo zilisitishwa. Kwa sasa nchi zote mbili zinaangazia uwezekano wa kufufua na kuboresho ufadhili huo kwa manufaa ya pande zote mbili.

Share: