Congo waziri mkuu jean michel ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Michel Sama Lukonde amejiuzulu, hatua inayosababisha kuvunjwa kwa Serikali yake, Waziri Mkuu huyo aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi siku nane baada ya kuidhinishwa kwa nafasi yake kama Mbunge wa kitaifa.

Mtandao wa DW Kiswahili umeripoti kuwa sasa Lukonde atahudumu Bungeni katika nafasi ya ubunge, Ofisi ya Rais imesema ombi lake la kujiuzulu limekubaliwa, hata hivyo Rais ameiomba Serikali ya Lukonde kuendelea kuyashughulikia masuala ya sasa hadi pale Serikali mpya itakapoundwa ingawa hadi sasa bado haijatoa sababu za kujiuzulu kwake.

Lukonde aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo yenye utajiri wa madini Februari 2021 akiwa na umri wa miaka 43 wakati huo.

Share: