
China yaanza kuwalipa wafanyakazi wanaoanzisha mahusiano
Makampuni kadhaa nchini China yameanzisha mpango wa kuwahamasisha wafanyakazi wao ambao hawako kwenye mahusiano kuanza kutengeneza mahusiano kwa kuwapa motisha ya pesa. Kupitia programu ya kuunganisha wapenzi, kila mfanyakazi anayefanikisha kukutana na mtu anayetambulika na kuthibitishwa, atalipwa dola 10 za Marekani.
Zaidi ya hayo, endapo mahusiano hayo yataendelea kwa muda wa miezi mitatu, wapenzi wote wawili pamoja na aliyewaunganisha hupokea zawadi ya dola 140 za Kimarekani.
Mpango huu unalenga kuboresha hali ya furaha na mshikamano wa wafanyakazi huku ukichangia katika kupunguza viwango vya chini vya ndoa na uzazi vinavyoikumba China kwa sasa.
Share: