China kutoa msaada baada ya taiwan kukumbwa na maafa ya tetemeko

Mamlaka ya Uchina imetoa taarifa mara baada ya tetemeko hilo kutokea, ikisema wako tayari kutoa msaada wa maafa.

Pwani ya mashariki ya Uchina iko kilomita 180 tu (maili 111) kutoka Taiwan.

"China ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali hiyo na inatoa pole za dhati kwa watu wa Taiwan walioathiriwa na maafa," alisema Zhu Fenglian, msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali.

Vyombo vya habari vya serikali ya China pia vimekuwa vikiripoti kwa wingi maafa hayo.China na Taiwan zina uhusiano wa wasiwasi.

Taiwan inajiona kuwa nchi huru, lakini Beijing inaona kuwa ni jimbo lililojitenga na ambalo hatimaye litakuwa sehemu ya nchi, na haijakataza matumizi ya nguvu kufanikisha hili.

Mvutano huo ni wa mara kwa mara - saa moja kabla ya tetemeko la ardhi wizara ya ulinzi ya Taiwan ilikuwa imetoa taarifa ya kila siku ikibainisha kuwa ndege 20 za kijeshi za China zilivuka katika eneo lake la ulinzi wa anga katika muda wa saa 24 zilizopita.

Share: