Cardi B ameahidi kutoa billion mbili kwa msanii Bia kama ataleta ushahidi wa yeye kucheat

Cardi B ametoa ofa ya dola milioni moja ((takribani shilingi bilioni 2.3) kwa rapa mwenzake BIA ikiwa ataweza kuthibitisha kwamba Cardi alimsaliti alyekuwa mume wake, Offset.

Hii inafuatia mstari wa BIA kwenye wimbo wake wa diss 'SUE MEEE?' ambapo aliimba, “Mwambie mume wako kwa sababu unapenda kudanganya kwenye viapo vyako.” Kava la wimbo huo linaonyesha screenshot ya tweet ya Offset akidai Cardi alimsaliti.

Cardi alikanusha madai hayo kupitia Twitter, akimjibu shabiki aliyesema BIA “amefichua kila kitu” kwa kusema, “Huyo m#### hajafichua chochote. Nitamlipa dola milioni moja pesa taslimu alete ushahidi wa mimi kuzungumza na mwanaume yeyote kabla ya hili kutoke!”

BIA alionekana kupuuza ofa hiyo kwa kujibu, “Boooo. Siko katika kiwango hicho. Jaribu mwingine tafadhali.”

Cardi B pia aliwahi kutishia kumshtaki BIA kwa kueneza uvumi huo, akidai kwamba ameenda mbali zaidi ya muziki kwa kujaribu kuvuruga familia yake.

Share: