Cag: mwaka wa fedha 2022/23 hakukuwa na huduma za kisaikolojia katika ngazi ya jamii

Hali hiyo ilichangiwa na ukosefu wa Fedha za kutosha kwa ajili ya huduma za Ustawi wa Jamii

Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi kwa mwaka wa fedha 2022/23 imebaini kutokuwepo kwa utambuzi wa watu wenye matatizo ya Afya ya Akili katika ngazi ya jamii badala yake utambuzi ulilenga watumiaji wa Dawa za Kulevya, Wazee, Walemavu, Watoto walio katika Mazingira Magumu, na waliopata Mimba za utotoni. Pia, hakukuwa na huduma za Kisaikolojia katika ngazi ya jamii. 

Hali hiyo ilichangiwa na ukosefu wa Fedha za kutosha kwa ajili ya huduma za Ustawi wa Jamii na kukosekana kwa Maafisa Ustawi katika ngazi za chini vikiwemo vijiji na mitaa. Pia, huduma za matunzo ya Kisaikolojia na usaidizi kutokuingizwa kikamilifu katika Mipango, Bajeti, Sera, Programu Afua, na Mikakati kwa ngazi zote za vituo vya Afya.

Share: