Burkina faso: baraza kuu la mawasiliano (csc) limetangaza kufungia matangazo na vipindi vya redio vya bbc africa na voa

Baraza Kuu la Mawasiliano (CSC) limetangaza kufungia Matangazo na vipindi vya Redio vya BBC Africa na VOA kufuatia kurusha ripoti ya Shirika la Human Rights Watch inayolishutumu Jeshi kwa kufanya udhalilishaji kwa Raia

Hatua ya CSC pia inahusisha kusimamishwa kwa matangazo ya Vituo hivyo kwa Wiki 2. Pia, tovuti na Mitandao ya Kidijitali ya BBC, VOA, na Shirika la Human Rights Watch zimefungiwa ndani ya Burkina Faso. 

Kwa Mujibu wa Ripoti ya HRW, Jeshi linadaiwa kuua Raia takriban 223 wakiweno Watoto 56 katika Vijiji vinavyoshutumiwa kushirikiana na Waasi. 

Share: