Bunge la taifa nchini kenya kuidhinisha shilingi bilioni 10.6 kwa ajili ya kukabiliana na dharura ya mafuriko na misaada

Kufikia Jumamosi zaidi ya watu 228 walikuwa wamefariki dunia kutokana na mafuriko na maelfu ya watu kujeruhiwa

Bunge la taifa nchini Kenya kuidhinisha shilingi bilioni 10.6 kwa ajili ya kukabiliana na dharura ya mafuriko na misaada ya kibinadamu kwasababu ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini humo.

Maelezo ya fedha hizo yapo kwenye bajeti ya II ya ziada katika kipindi cha mwaka wa fedha mwaka 2023/2024.

Kufikia Jumamosi zaidi ya watu 228 walikuwa wamefariki dunia kutokana na mafuriko na maelfu ya watu kujeruhiwa huku wengine wengi wakilazima kuhama makazi yao.

Mvua hiyo isiyokoma imeharibu mazao na mali huku serikeli ikitenga makazi ya muda kwa watu waliohama makwao.

Hatua hii inafuatia tangazo ya mamlaka ya hali ya hewa la kunyesha kwa mvua kubwa katika maeneo mengi kote nchini humo.





Share: