Hii wanafaa kukubaliana mapema kabla ya ndoa kufungwa
Bunge la Rwanda linajadili muswada ambao utawawezesha wanaotaka kufunga ndoa kupata haki ya kuchagua ni sehemu gani ya mali zao watakusanya pamoja au kutenganisha.
Hii wanafaa kukubaliana mapema kabla ya ndoa kufungwa, alisema Waziri wa Jinsia na Familia nchini Rwanda, Valentine Uwamariya akiwa bungeni.
Uwamariya anaelezea kuwa kuna taratibu tatu za mali katika ndoa.
Kuna ile inayohitaji mali kujumuishwa, ambayo ni mkataba ambao wanandoa huchagua umiliki wa pamoja wa mali zao zote.
Pia kuna mali ambayo washirika huchangia kila kitu wanachojenga kutoka siku ya harusi yao.
Ya tatu ni mgawanyo wa mali unaomaanisha mgawanyo kamili wa mali husika za wenye ndoa, bila usawa wowote wa faida iliyopatikana pindi ndoa yao inaisha.
Mbali na kukubaliana kuhusu mali wanayokusanya, na kile wanachotenganisha baada ya ndoa chini ya utawala mpya, muswada huu unapendekeza wapenzi kukubaliana nini kitafanyika katika kesi ya talaka.
Hii itahusisha jinsi watakavyogawana mali inayomilikiwa kwa pamoja, au jinsi mali zingine zitakavyothibitiwa wakati mmoja wao anapokufa.