Bunge la kenya linatarajiwa kupiga kura kuhusu mswada mpya wa fedha bungeni

Bunge la Kenya linatarajiwa kupiga kura kuhusu mswada mpya wa fedha bungeni, huku baadhi ya raia wa nchi hiyo wengi wao wakiwa vijana wakiandamana kuupinga.

Maandamano ya kuupinga muswada huo ambayoyalianza Jumanne wiki hii yamesababishwa kukamatwa kwa makumi ya watu katika mji mkuu wa Nairobi wakati wakiandamana kupinga mswada mpya wa fedha.

Licha ya mji mkuu Nairobi maandamano haya yamefanyika katika miji mingine mbali mbali ya nchi hiyo.

Wanasheria na makundi ya haki za binadamu wameishutumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani.

Mapema siku ya Jumanne serikali ya Kenya iliunga mkono kwa sehemu madai ya waandamanaji na kutangaza kufuta baadhi ya kodi ikiwemo kodi ya mkate.

Rais William Ruto anasema fedha zaidi zinastahili kukusanywa kupitia ushuru ili kupunguza deni la taifa la zaidi ya dola bilioni sabini.

Share: