Boeing yakiri makosa ya kuanguka kwa mlango wa ndege ikiwa angani

Bosi wa kampuni ya Boeing amekiri kuwa mtengenezaji huyo wa ndege alikuwa na makosa baada ya moja ya ndege zake kulipuliwa na mlango muda mfupi baada ya kupaa nchini Marekani.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati mlango ambao haujatumiwa ulipasuka kutoka kwa ndege ya Alaska Airlines kutoka Portland, Oregon siku ya Ijumaa.

Marekani imesimamisha ndege 171 kati ya Boeing 737 Max 9 tangu kutokea kwa tukio hilo.

Siku ya Jumanne, rais na affina Mkuu mtendaji wa Boeing Dave Calhoun alisema kampuni hiyo "inakubali makosa yetu".

"Plagi" ya mlango ambayo ilianguka kutoka kwa ndege ilikuwa na uzito wa kilo 27 (lb 60) na ilitumiwa kuizba njia ya dharura ambayo ilijengwa ndani ya ndege, lakini haikuhitajika na Alaska Airlines.

Sehemu iliyopotea ya ndege ilitolewa kutoka kwa bustani nyuma ya nyumba ya mwalimu wa Portland, kulingana na Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri wa Marekani (NTSB)

Share: