
Bilionea mwanzilishi mwenza wa Microsoft, Bill Gates, amesema kuwa maendeleo ya akili bandia (AI) katika miaka kumi ijayo yatafanya binadamu wasihitajike tena kwa kazi nyingi ulimwenguni.
Akizungumza katika mahojiano na Jimmy Fallon kwenye kipindi cha The Tonight Show mwezi Februari, Gates alieleza kuwa kwa sasa kuna uhaba wa wataalamu katika sekta mbalimbali kama vile udaktari na elimu. Hata hivyo, aliendelea kusema kuwa AI itafanya huduma bora za matibabu na ufundishaji kuwa nafuu na kupatikana kwa urahisi kwa kila mtu.
Kauli hii inasisitiza jinsi teknolojia inavyobadilisha mfumo wa kazi duniani, huku AI ikionekana kuchukua nafasi kubwa ya binadamu katika maisha ya kila siku.
Share: