Bilionea maarufu wa korea kusini chey tae-won amemriwa kumlipa kumlipa mtalaka wake dola bilioni 1

Mfanyabiashara na Bilionea Maarufu wa Korea Kusini, Chey Tae-won amemriwa kumlipa mtalaka wake zaidi ya dola bilioni moja katika kesi ya talaka kubwa kuliko zote kuwahi kutokea nchini humo.

Hukumu hiyo inakuja takribani miaka 10 tangu ndoa ya wawili hao ilipovunjika baada ya kugundulika kuwa bilionea huyo alizaa na mpenzi wake nje ya ndoa.

Mahakama kuu ya Seoul imesema kuwa Bi.Roh So-young, aliyekuwa mke wa bilionea huyo kwa miaka 35 ana haki ya kupata sehemu ya shea za kampuni ya SK group inayomilikiwa na bilionea huyo.

Share: