Bashungwa aagiza mameneja wa tanroads kukarabati mifereji ya barabara.

Serikali inajipanga kutafuta namna ya kuwaondolea adha ya mafuriko wananchi katika barabara ya Mwenge - Bagamoyo.

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amewaagiza Mameneja wa Mikoa wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mikoa yote nchini kukarabati mifereji iliyo pembezoni mwa barabara kuu ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua ikiwemo kuharibika kwa barabara.

Bashungwa ametoa agizo hilo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta aliyeuliza kuhusu ni lini Wizara Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi itasafisha mifereji iliyozibwa wakati wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo. 

Aidha, Bashungwa amesema Serikali inajipanga kutafuta namna ya kuwaondolea adha ya mafuriko wananchi katika barabara ya Mwenge - Bagamoyo. 

Naye, Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima alitaka kujua ni lini ujenzi wa barabara ya Mabasi yaendayo haraka inayoanzia Mwenge - Tegeta - Basihaya itaanza kujengwa. 

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya amesema hatua iliyopo kwa sasa ni hatua ya awali kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo na tayaru mkandarasi yupo eneo la ujenzi.

Share: