Basata ya sisitiza wasanii kujikita katika maombolezo ya hayati ally hassan mwinyi

Taarifa ya BASATA imesema Baraza hilo linaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa Rais Samia na Rais wa Zanzibar Dr. Mwinyi

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limewasihi Wasanii na Wadau wa sanaa na burudani hususani katika Kumbi za burudani, starehe na matamasha Nchini kujikita katika maombolezo kwa kipindi hiki cha siku saba za maombolezo zilizotangazwa na Rais Samia kufuatia kifo cha Rais mstaafu Hayati Ally Hassan Mwinyi.

Taarifa ya BASATA imesema Baraza hilo linaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa Rais Samia na Rais wa Zanzibar Dr. Mwinyi, kufuatia kifo cha Rais huyo mstaafu.

“Kufuatia hali hiyo, sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa namba 23 ya mwaka 1984 na marekebisho yake ya mwaka 2019, inatoa Mamlaka kwa Baraza la Sanaa la Taifa kusimamia na kuendelea sekta ya sanaa na burudani Nchini hivyo Baraza linawasihi Wasanii na Wadau wa sanaa katika kumbi za burudani, starehe na matamasha kujikita katika maombolezo kwa kipindi cha siku saba zilizotangazwa na Mhe. Rais ili kuwafariji Wanafamilia na Watanzania” imeeleza taarifa ya BASATA.

“Baraza linawasihi Wasanii na Wadau wa sanaa kutumia kipindi hiki kutafakari mchango wake katika maendeleo ya Nchi yetu ikiwemo sanaa” - taarifa ya BASATA iliyotolewa na Katibu Mtendaji Dr. Kedmon Mapana imemalizia.

Share: