Baridi kali na barafu yasababisha umeme kukatika ukraine

Hali ya baridi na upepo mkali pamoja na barafu imesababisha kukatwa kwa nguvu za umeme katika makaazi 1,025.

Wasimamizi wa gridi ya kusambaza umeme nchini Ukraine wamesema hali mbaya ya hewa ya baridi kali imesababisha zaidi ya miji na vijiji 1000 kukosa umeme katika mikoa tisa ya nchi hiyo.

Shirika la umeme Ukrenegro limewatolea mwito wananchi kutumia vizuri umeme kipindi hiki ambapo mfumo wa usambazaji umeme umedhoofishwa na mashambulizi ya Urusi.

Shirika hilo limetanabahisha kwamba matumizi ya umeme yalikuwa yamefikiwa viwango vya juu kabisa wiki hii kutokana na kushuka kwa viwango vya joto katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Hali ya baridi na upepo mkali pamoja na barafu imesababisha kukatwa kwa nguvu za umeme katika makaazi 1,025.

Share: