Baraza la mitihani tanzania (necta) latangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita 2024

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Mei mwaka huu 2024 ambapo jumla ya Watahiniwa 111,056 wa Shule na kujitegemea sawa na 99.43% ya Watahiniwa wenye matokeo ya mtihani huo wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo leo Visiwani Zanzibar, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr. Said Mohamed, amesema “Wanawake waliofaulu ni 49,837 sawa na 99.61% wakati Wanaume waliofaulu ni 61,219 sawa na 99.28%, mwaka 2023 Watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 104,549 sawa na 99.23%, hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa 0.20% ikilinganishwa na mwaka 2023”

Share: