Baraza la mawaziri linaloongozwa na waziri mkuu nchini israeli limeunga mkono serikali kufungia kituo cha televisheni cha al jazeera

Serikali imefikia uamuzi huo ikidai Kituo hicho kinachofadhiliwa na Serikali ya Qatar kimekuwa kikiripoti Habari ambazo zinatishia Usalama wa Taifa

Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu limepiga Kura na kuunga mkono uamuzi wa Serikali kufungia shughuli zote za Kituo cha Televisheni cha Al Jazeera kwa muda wote wa Vita kati ya Israel na Wanamgambo wa Hamas.

Kwa mujibu wa taarifa ya Netanyahu, Serikali imefikia uamuzi huo ikidai Kituo hicho kinachofadhiliwa na Serikali ya Qatar kimekuwa kikiripoti Habari ambazo zinatishia Usalama wa Taifa, ingawa Al Jazeera inaweza kupinga uamuzi huo kupitia Mahakama

Aidha, kufungiwa kwa Al Jazeera kunakuja ikiwa ni saa chache tangu Serikali ya Israel ikatae kusitisha mashambulizi katika eneo la Gaza huku Waziri Mkuu Netanyahu akidai kusitisha Vita itakuwa sawa na kuwaogopa Hamas

Share: