Kila mauzo ya ndege za kivita yatahitaji idhini ya baraza la mawaziri, mamlaka ilisema.
Baraza la mawaziri la Japan limeidhinisha mauzo ya nje ya ndege mpya za kivita inazotengeneza na Uingereza na Italia, katika hatua ya hivi punde zaidi ya kuachana na sera zake za kuunga mkono jitihada za kuafikiaamani.
Ilirahisisha sheria za usafirishaji wa silaha kuruhusu ndege hizo kuuzwa kwa nchi ambazo Japan imetia saini mikataba ya ulinzi, na ambapo hakuna mzozo unaoendelea.
Japan imeahidi kuongeza maradufu matumizi ya kijeshi ifikapo mwaka 2027, ikitaja vitisho vinavyotolewa na China na Korea Kaskazini.
Kila mauzo ya ndege za kivita yatahitaji idhini ya baraza la mawaziri, mamlaka ilisema.
Mnamo Desemba 2022, Japan iliingia katika ushirikiano wa Uingereza na Italia, unaoitwa Tempest, ili kuunda ndege hii mpya ya kivita ambayo itatumia akili mnembana vihisi vya hali ya juu kuwasaidia marubani.
Jeti hizo zinatarajiwa kutumwa ifikapo 2035 - katika ule ambao ni ushirikiano wa kwanza wa Tokyo wa kutengeneza vifaa vya ulinzi na nchi nyingine isipokuwa Marekani.
Hatua ya hivi punde inakuja kabla ya ziara rasmi ya Waziri Mkuu Fumio Kishida nchini Marekani mwezi Aprili, ambapo anatarajiwa kusisitiza ushirikiano wa Tokyo na Washington na utayari wa nchi yake kuhusika zaidi katika ushirikiano wa ulinzi.