Imeelezwa kuwa hatua hiyo imefikiwa ili kuhakikisha Wanataaluma watakaopatikana wanakuwa ni wenye sifa na weledi
Baraza la Famasi Tanzania limefuta Matokeo yote ya Watahiniwa waliofanya mitihani ya Leseni ngazi ya Fundi Dawa Sanifu iliyofanyika February 2024 baada ya kuthibitika kulikuwa na udanganyifu
Imeelezwa kuwa hatua hiyo imefikiwa ili kuhakikisha Wanataaluma watakaopatikana wanakuwa ni wenye sifa na weledi katika viwango vilivyowekwa kabla ya kusajiliwa na kutoa huduma za dawa ili kulinda Afya na usalama wa Wagonjwa
Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza hilo, Watahiniwa hao watalazimika kurudia mtihani hiyo July 2024 bila malipo ambapo Watahiniwa watafanyia Mitihani katika Vituo vya awali kwa namba mpya watakazotumiwa bila kujisajili upya
Share: