Balozi hassani iddi mwamweta balozi wa tanzania nchini ujerumani amewasilisha hati za utambulisho kwa rais wa shirikisho la uswisi

Balozi Hassani Iddi Mwamweta ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, amewasilisha Hati za Utambulisho (letters of Credence) kwa Mhe. Viola Amherd, Rais wa Shirikisho la Uswisi. 

Hatua hii inamfanya kuwa Balozi wa Tanzania mwenye makazi Berlin, Ujerumani.

Pamoja na kuwasilisha salamu za upendo kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Balozi Mwamweta aliishukuru Serikali ya Uswisi kwa namna inavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inalenga kuwaletea maendeleo Watanzania hususan miradi ya elimu na afya.

Balozi Mwamweta ameomba ushirikiano zaidi kutoka Serikali Uswisi ili kupata matokeo mazuri kwenye maeneo ya vipaumbele vya Tanzania ambayo ni pamoja na utalii; biashara na Uwekezaji; elimu na afya.

Mahusiano baina ya Tanzania na Uswisi ni mazuri na ya kihistoria. 

Pamoja na Uswisi, Balozi Mwamweta anaiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani, Poland, Holy See, Czech, Slovakia, Burgaria, Romania na Hungry.

Share: