Ausc yapendekeza kubuniwa kwa kikosi kipya cha muda kitakachosaidia vikosi vya usalama ndani ya somalia

Somalia tayari imeshatuma maombi kwa UNSC kutaka kikosi cha umoja wa mataifa UNISOM

Baraza la usalama la Umoja wa Africa AUSC limependekeza kubuniwa kwa kikosi kipya cha muda kitakachosaidia vikosi vya usalama ndani ya Somalia kujiandaa kulinda taifa hilo, baada ya kikosi kilichoko sasa cha mpito ATMIS kukamilisha muda wake wa kuhudumu nchini humo.

Katika kikao kilichofanyika mjini Addis Ababa Juni 21, baraza hilo kimeafikia kwamba kuna haja ya kikosi cha ATMIS kubadilishana mamlaka na kile kipya ambacho kitatangazwa hivi karibuni, ili kuendeleza majukumu yake bila tatizo.

ATMIS ambayo ilibuniwa 2022, inatarajiwa kukamilika Desemba 2024, huku tayari wanajeshi 3000 wakiwa wameshaondoka Somalia. Awamu ya nne ya kupunguza wanajeshi hao inaanza Juni 2024 ambapo wanajeshi 2000 wanatarajiwa kuondoka Somalia na kambi walizosimamia kukabidhiwa wanajeshi wa Somalia. Ifikapo Desemba, wanajeshi wengine 2000 wanatakiwa kuondoka.

Mojawapo ya majukumu kuu ya kikosi kitakachoingia SOMALIA baada ya ATMIS kuondoka , ni kusaidia vikosi vya usalama vya Somalia kukabiliana na tishio la usalama wa nchi hiyo.

Lakini kabla ya mwisho wa 2024 AU inatarajiwa kutuma maombi kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuweka mipango ya kufadhili kikosi kipya na cha sasa.

Somalia tayari imeshatuma maombi kwa UNSC kutaka kikosi cha umoja wa mataifa UNISOM kinachosaidiana na ATMIS kulinda usalama nchini humo kuondoka ifikapo mwishoni mwa 2024.

Share: