Askofu kardinali polycarp pengo amefika ofisini kwa mkuu wa mkoa wa arusha mh. paul christian makonda leo aprili 15, 2024

Askofu mstaafu Kardinali Pengo akiambatana na Viongozi wengine wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, wamemuombea kheri na baraka Mh. Paul Makonda

Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Dar Es salaam Kardinali Polycarp Pengo leo Aprili 15, 2024 amefika ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Paul Christian Makonda, Kuzungumza naye na kumuombea Kheri Katika kuwatumikia wananchi wa Arusha.


Kando ya Mazungumzo yao, Askofu mstaafu Kardinali Pengo akiambatana na Viongozi wengine wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, wamemuombea kheri na baraka Mh. Paul Makonda na Kumuhimiza Kuendelea kujitoa katika kuwatumikia Wananchi anaowangoza kama Mapenzi na Matakwa ya Mwenyenzi Mungu yanavyohimiza kujitoa kwa wengine.

Kardinali Polycarp Pengo katika maisha yake ya Utume kama Padre na Askofu, anasifika kwa uimara wake katika masuala ya Imani, maadili na Utu wema, akitajwa kama chombo na shuhuda wa majadiliano ya Kidini, kisiasa na kitamaduni, mambo yaliyosaidia kujenga na kuimarisha Maridhiano, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Kanisa katoliki duniani linamtaja Askofu mstaafu Kardinali Pengo kama kiongozi mwenye kuthamini sana vijana, kuwekeza amana, utajiri, uzoefu na Mang'amuzi yake katika Malezi na ustawi wa Vijana.

Share: